Beki anaesemekana kuachwa na Wekundu Wa Msimbazi Simba, Juuko Murshid amejumuishwa katika kikosi cha mwisho cha Uganda cha wachezaji 19 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe kesho.

Kikosi cha The Cranes kimeondoka leo asubuhi mjini Entebe kuelekea mjini Harare kwa mchezo wa kirafiki na wenyeji, Zimbabwe kabla ya kumenyana na Botswana katika mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwishoni utakaochezwa mwishoni mwa juma hili.

Katika kikosi hicho, Micho amemjumuisha pia mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anachezea SonderjyskE ya Denmark.

Kikosi kamili cha The Cranes kinaundwa; Denis Onyango, Robert Odongkara, Denis Iguma, Joseph Ochaya, Luwagga Kizito, Okwi Emma, Wasswa Hassan Mawanda, Juuko Murushid, Sekisambu Erisa, Kasirye Davis, Massa Geoffrey, Miya Faruku, Lorenzen Melvyn, Walusimbi Godfrey, Aucho Khalid, Lubega Idrisa,  Isinde Isaac, Tony Mawejje na Yassar Mugerwa.

Borussia Dortmund Wakanusha Kuondoka Kwa Aubameyang
Jose Mourinho Ampigia Debe Rio Ferdinand