Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus FC wamekataa ofa ya Pauni milioni 85, iliyowasilishwa na klabu ya Man Utd kwa ajili ya usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa, Paul Labile Pogba.

Man Utd waliwasilisha ofa hiyo kwa kuamini watafanikisha mpango wa kumnasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini imekua tofauti kutokana na uongozi wa Juventus kusimamia kauli waliyoitoa juma lililiopita.

Juventus walitoa kauli ya kuwa tayari kumuachia Pogba kuondoka mjini Turin, kwa kitita cha Pauni milion 100 ambacho wanaamini ndio thamani sahihi kwa mchezaji huyo kwa sasa.

Mapema hii leo kituo cha televisheni cha nchini Italia cha Sky Italy, kimeripoti kwamba, huenda Man Utd wakawasilisha ofa nyingine, kufuatia mtendaji mkuu wa klabu hiyo ya Old Trafford, Ed Woodward kuonyesha kutokukata tamaa.

Mashabiki Wa Arsenal Wapingana Na Babu Wenger
Rafael Benitez Aitega Liverpool