Mabingwa wa zamani wa Italia klabu ya Juventus wanaongoza katika harakati za kumuwania kiungo kutoka Ufaransa na Manchester United, Paul Pogba ambaye ataondoka Old Traffold mwishoni mwa msimu huu 2021/22.

Pogba ameripotiwa kuwa mbioni kuondoka Manchester United, kufuatia kugoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo, hali ambayo imezifanya klabu kadhaa kuanza kumnyatia.

Miongoni mwa klabu zinazotajwa na kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 ni Real Madrid (Hispania), Juventus (Italia) na Paris Saint-Germain (Ufaransa).

Hata hivyo, uwezekano wa Pogba kurejea Italia kujiunga tena na Juventus ni mkubwa, ambapo klabu hiyo inaweza kuwa katika mipango inayotajwa kuongoza mbio za kuinasa saini yake kwa mujibu wa Rudy Galetti.

Wakati Pogba akipigiwa upatu kurejea Juventus, uongozi wa klabu hiyo unajiandaa kumuuza mchezaji wa zamani wa Arsenal, Aaron Ramsey pamoja na Weston McKennie au Adrien Rabiot ili kumudu gharama ya mkataba wa Euro Milioni 12 kwa msimu, pamoja na Bonasi kwa mchezaji huyo wa ‘Mashetani Wekundu’.

Pogba alisajiliwa Manchester United Agosti 08, 2016 akitokea Juventus, kwa ada ya Pauni Milioni 83.6.

Vinicius Junior kusaini mkataba mpya Bernabeu
Kuna mgao wa Umeme?:Spika Ndugai