Mshambuliaji kutoka nchini Croatia, Marko Pjaca anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji waliosajiliwa na mabingwa wa soka nchini Italia (Serie A), Juventus katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Tayari mabingwa hao Scudetto wameshafanikisha usajili wa Dani Alves akitokea FC Barcelona, Miralem Pjanic akitokea AS Roma pamoja na Medhi Benatia kutoka FC Bayern Munich kwa mkopo.

Pjaca anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kutoka kwenye klabu ya  Dinamo Zagreb ndani ya juma hili, baada ya taratibu zote za mazungumzo kukamilishwa na viongozi wa pande zote mbili.

Euro milioni 25 zinatajwa kuwa ada ya uhamisho wa Pjaca ambaye alionyesha uwezo mkubwa wakati wa fainali za Euro 2016 ambazo zilifikia tamati Julai 10 nchini Ufaransa.

Katika hatua nyingine mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ameanza kuwaaga mashabiki wake wa nchini Croatia kupitia mitandao ya kijamii, hali ambayo imeongeza chachu ya kuamini safari yake ya kuanza maisha mapya huko nchini Italia imekaribia.

“Ningependa kuwashukuru watu wote waliokua karibu yangu kwa wakati wote, na sina budi kuwashukuru wachezaji wenzangu wa Dinamo Zagreb”

“Mimi ni kijana wa Zagreb ninaipenda na nitaendelea kuipenda Dinamo, na daima nitaendelea kuyakumbuka mazuri niliyoyafanya hapa.” Pjaca ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Pjaca alisajiliwa na klabu ya Dinamo Zagreb mwaka 2014 akitokea NK Lokomotiva Zagreb, kwa ada ya uhamisho ya Euro milion moja, na mpaka sasa yu njiani kuondoka amecheza michezo 100 ya ligi ya nchini Croatia na kufunga mabao 28.

Inauma: Atumiwa zawadi ya picha za mkewe akifanya ngono kinyume na maumbile, Wasikilize Mke na Mume hapa
Maafande Wa Ruvu Shooting Waachana Na Tom Olaba