Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wapo tayari kumuuza kiungo wao kutoka Ufaransa Paul Pogba ambaye anatakiwa na klabu ya Man Utd ya England.

Ukurasa wa mbele wa gazeti la la Stampa la nchini Italia umeelza kwamba, Juventus wamewawashia taa ya kijani Man Utd baada ya kukutana na wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, Mino Raiola.

Taarifa hizo zimeongeza kwamba, Juventus wametoa masharti ya kumuuza Pogba endapo Man Utd watakuabli kutoa kiasi cha pauni milion 100 kama ada ya usajili ya mchezaji huyo, ambaye jana alikua sehemu ya kikosi cha Ufaransa ambacho kilishindwa kutwaa ubingwa wa Ulaya mbele ya mashabiki wa soka waliokua wamafurika kwenye uwanja wa Stade de France, kwa kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa ya Ureno.

Hata hivyo bado upande wa Man Utd, haujazungumza suala lolote kuhusu ruhusa iliyotolewa na uongozi wa Juventus ya kukubalia Pogba aondoke mjini Turin na kurejea Old Trafford, japo baadhi ya tetesi wa mustakabli wa mkataba wa kiungo huyo kuanza kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari.

Inaelezwa kwamba endapo dili hilo litakamilishwa, Pogba atasaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu ya Man Utd, ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milion 75 kwa mwaka.

Juve wameonyesha kuwa tayari kufanya biashara hiyo, huku wakihusishwa na mipango ya kuwa tayari kuzipa pengo la Pogba kwa kumsajili kiungo wa klabu ya Dinamo Zagreb ya nchini Croatia, Marko Pjaca.

Pogba alilelewa na kukuzwa na kikosi cha Man Utd, baada ya kusajiliwa akiwa na umri wa miaka 16, akitokea nchini kwao Ufaransa katika kituo cha Le Havre, lakini ilipofika mwaka 2012, aliondoka klabuni hapo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilichokua kikinolewa na babu Sir Alex Ferguson .

Waarabu Kuchezesha Young Africas Vs Medeama
Mtoto wa Osama aitumia Marekani Ujumbe kuhusu mpango wa kulipa kisasi