Huenda ikawa taarifa mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao walianza kuamini taratibu za uhamisho wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya SSC Napoli, Gonzalo Higuain.

Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wameingia katika dili la kutaka kumsajili mshambuliaji huyo na wakati wowote huenda wakapewa ruhusa ya kuzungumza nae, kuhusu maslahi binafsi.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger mwanzoni mwa juma hili aliripotiwa kuwa katika harakati za kufikiria kumtoa mshambuliaji wake kutoka nchini Ufaransa Olivier Giroud, ili awe sehemu ya mpango wa usajili wa Higuain.

Gonzalo Higuain01Gonzalo Higuain

Taarifa za awali ambazo zimeripotiwa katika tovuti ya Goal, zimedai kwamba Juventus wapo tayari kumpa mkataba wa miaka minne mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milioni 7 kwa kila mwaka.

Kama Juventus watafanikisha azma ya kumsajili Higuain, itakuwa ni mara ya pili kwa Arsene Wenger kushindwa kufikia lengo tangu msimu wa 2015-16 ulipofikia tamati mwezi Mei.

Wenger alipanga kumsajili mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini England, Leicester City, Jamie Vardy lakini alishindwa kutokana na uongozi wa klabu hiyo kufanikisha mpango wa kumsainisha mkataba mpya.

Neven Subotic Anuakia Riverside Stadium
Audio: "Chadema Wameniomba Nigombee Nafasi Hii.., Sikuwa na Ugomvi Mkubwa na CCM..." - Sumaye