Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, wameipa kisogo klabu ya Chelsea ambayo ilionyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kati Leonardo Bonucci, na badala yake wametoa ruhusa kwa Manchester City kukamilisha mpango huo.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti la michezo la nchini Italia (Gazzetta dello Sport) zinaeleza kwamba, beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ameshafanya mazungumzo binafsi na uongozi wa Man City na kufikia makubaliano ya malipo yake ya mwaka.

Gazeti hilo limefafanua kwamba pande hizo mbili zimefikia pazuri baada ya kukubaliana malipo ya Euro milion 8 kwa mwaka kama mshahara.

Kiasi hicho cha mshahara kitakua na ongezeko la Euro milion 2, kutokana na malipo ya sasa ya Bonucci kuwa ni Euro milion 6 anazolipwa na Juventus kwa mwaka.

Hata hivyo kazi iliyosalia katika usajili wa Bonucci, ni makubaliano kati ya Man City na Juventus.

Man City wamejipanga kumsajili Bonucci kwa kiasi cha Euro milion 60.

Chelsea walianza mpango wa kutaka kumsajili Bonucci, mara baada ya kuingia mkataba na meneja wao mpya kutoka nchini Italia, Antonio Conte lakini harakati hizo zinaonekana kuingia gizani kutokana na ukimya uliotawala

Polisi kuwasaka wafanyakazi wenye vyeti feki, ‘tutamnyofoa mmojammoja’
Mahakama yawarudisha kizimbani Wasira, Esther Bulaya kugombea ubunge