Baada ya kuripotiwa kuwepo kwa mazungumzo ya faragha mwishoni mwa juma lililopita baina ya viongozi wa klabu bingwa nchini Italia, Juventus dhidi ya viongozi wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona huko mjini Milan kuhusu mipango ya usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba, hali si shwari.

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Juventus, Giuseppe Marotta ambaye anadaiwa alikutana na mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona, Ariedo Braida mjini Milan na kupata chakula cha jioni siku ya jumapili, amesema wameikataa ofa ya Barca ya Euro million 80.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye magazeti ya Diario Sport pamoja na Mundo Deportivo, imeelezwa kwamba viongozi hao walikutana tena kwa mara ya pili hapo jana na kutoafikiana juu ya ofa ambayo FC Barcelona ambayo waliamini huenda ingewasaidia kumng’oa Paul Pogba Juventus Stadium.

Hata hivyo usiku wa kuamkia hii leo Marotta alifanyiwa mahojiano na muandishi wa habari wa gazeti la michezo la nchini Italia liitwalo Gazzetta dello Sport na kukanusha taarifa ambazo zilikua zimeshaanza kusambaa kwa kuelezwa kwamba tayari Juventus walikua wameikubali ofa hiyo ya Euro million 80.
Marotta amesema hawakukubaliana na ofa hiyo na amesisitiza wazi kwamba FC Barcelona wanatambua thamani ya Pogba hivyo kama wanahitaji mazungumzo yaendelee baina yao watapaswa kufuata njia inayostahili.

Pogba amekua akihusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na baadhi ya klabu nguli barani Ulaya, lakini FC Barcelona wanaonekana kupewa kipaumbele katika mkakati huo, tofauti na PSG, Chalesea pamoja na Man City.

Ray C Anatafuta Mume Wa Kuishi Nae Milele, Ataja Sifa
Ngoja Ngoja Za Man Utd, Arsenal Zawapa Nafasi BVB