Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wamepania kuzibwaga Manchester United na Arsenal katika vita ya kumuwania mshambuliaji kutoka nchini Uruguay na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), Edinson Cavani.

Cavani mwenye umri wa miaka 29, kwa mara nyingine ameingia kwenye rada za mabosi wa Juve baada ya kushindwa kupata saini yake miaka mitatu iliyopita.

Mshambuliaji huyo atafungasha kila kilicho chake mwishoni mwa msimu huu na kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake, baada ya meneja wa PSG Laurent Blanc kueleza hadharani kutomuhitaji tena.

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la nchini Italia (Gazzetta dello Sport) inadaiwa kuwa Juventus wako tayari kulipa pauni milioni 35 kama asda ya usajili wa Cavani.

Ada hiyo inatarajiwa kuwa na utofauti mkubwa dhidi ya zile ambazo zimeandaliwa na klabu za nchini England, Arsenal na United.

Wakati Juventus wakitamba kumfanya Cavani kuwa mchezaji ghali zaidi katika kikosi chao, Man Utd wapo tayari kumlipa mshahara wa pauni milioni 5.4 kwa msimu, huku Arsenal ikielezwa kutokuwa na uwezo wa kutokidhi mahitaji ya PSG.

Juventus ilijaribu kumnasa bila mafanikio Cavani mwaka 2013 baada ya kuiongoza SSC Napoli ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Serie A, ambapo mshambuliaji huyo aliibuka kinara wa ufungaji kwa kufunga mabao 29 kabla ya kuhamia PSG.

Ronaldo Afichua Siri Nzito Iliyodumu Kwa Miaka Minane
Mourinho Aendelea Kutoa Maelekezo Man Utd