Msanii wa RnB Juma Jux amesema hawezi kumuongelea vibaya aliyekuwa mpenzi wake  Vanessa Mdee hata kama wameachana na kila mmoja anfanya mambo yake.

Jux amesema licha ya kuachana kwao bado wapo sawa pia hajamu”unfollow” Vannessa mdee kwenye mitandao ya kijamii

“Sioni sababu ya kumongelea vitu vibaya na kwanini nifanye hivyo na nisiongee vitu vizuri,  kwenye vitu vibaya na vizuri huwa nachagua vizuri siku zote, hayo ni maamuzi ya mtu au malezi ya mtu kwa sababu nimeshakuwa katika matukio mazuri na yeye kipindi cha nyuma na zilikuwa bora zaidi kuliko kipindi hiki” amesema Jux alipoongea na EATV.

Wawili hao wameachana miezi kadhaa iliyopita, ambapo sasa hivi kila mtu yupo katika mahusiano mapya, icha ya mashabiki kutaka mahusiano hayo yaendelee.

 

Lampard 'akomalia' mapambano kwa vigogo Uingereza
China yamuweka kitimoto balozi wa Marekani