Serikali imewataka wananchi wa Tanzania kujihusisha na ulinzi na usafi wa nchi bila kujali kazi hiyo inafanywa kwa ufanisi na Jeshi la Wananchi.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema hayo alipozungumza na Dar24 katika mahojiano Maalumu ambapo alikua akizungumzia mahusiano ya wananchi na Jeshi la Wananchi.

Dkt. Stergomena amesema kuwa kazi ya kulinda nchi ni ya wananchi kwanza ndio wanafuata Wanajeshi pamoja usaffi wa Jiji kuwa iko siku watawapa wanajeshi ilio Jiji live safi na kuanzia hapo wananchi washike kasi.

“Ninachokiona mahusiano ni mazuri sana, kwa sababu wananchi wanaliamini jeshi lao, wanaliona linafanya shughuli zake vipi, wanaliamini, na pia katika huduma za kijamii tuna hospitali zipo maeneo tofauti, na wengi wanaohudumiwa humo ni wananchi,” amesema Dkt. Stergomena.

Dkt. Stergomena amewataka wananchi kuwasaidia wanajeshi katika kutimiza majukumu yao hasa kuanzia malezi ya watoto kwa kuwa ulinzi wa Nchi sio kazi ya Wanajeshi peke yao bali kazi ya wananchi wote.

“Ni Kweli kwamba kunakua na Uoga kwa sababu hata wazazi wanachangia watoto kuogopa wanajeshi, mtoto anaambiwa unamuona yule mwanajeshi ntamwita aje, kumbe wazazi wanatakiwa kuwaaminisha watoto kuwa mwanajeshi ni mlinzi wa taifa leu hivyo amsaidie kutimiza majukumu yake,”

“Ulinzi wa nchi yetu ni kazi yetu sote, uwe raia au mwanajeshi una jukumu la kulinda kwa hiyo toa ushirikiano kwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ili wafanye kazi kwa faida yetu sote.” Ameongeza.

Kuhusiana na swala usafi ambapo mara kadhaa Jeshi lkimekua likihusika kushiriki usafi katika harambee tofauti na hasa katika maeneo yao ya makazi, Dkt. Stergomena amesema kuwa wananchi wote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya usafi.

“Nidhamu inaanzia mbali Sana, ianzie kwenye familia, ifundishwe mashuleni, ianzie kwenye jamii ili wewe mwenyewe ukipita pale uone kuwa pale nimepapenda hivyo uhusike kusafisha maeneo yako na nchi nzima,” amesema Dkt. Stergomena.

Manara awakumbusha wachezaji Young Africans
KMC FC yaanza kuisaka Mtibwa Sugar