Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati kupitia programu ya ‘Peoples Empowerment Foundation’ chini ya Kampuni ya Camal Group amewakabidhi viungo bandia walemavu kumi wa miguu kutoka wilaya tofauti za mkoa huo.
 
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ofisi ya Mbunge huyo ambapo amesema kuwa Mh. Ritta Kabati alifanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Iringa na kubaini uwepo wa walemavu zaidi ya 110 wa viungo mbalimbali vya mwili.
 
Mratibu huyo wa Mbunge Kabati amesema kuwa zoezi la kuwakabidhi walemavu hao viungo bandia lilifanyika Januari 20 mwaka huu Jijini Dar es laam na lilidhaminiwa na kampuni ya Camal Group. Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Kazi Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa.
 
“Mbunge alifanya ziara katika mkoa wa Iringa ndipo alipobaini uwepo wa hawa hatu wenye mahitaji maalumu tuliwapata watu zaidi ya 110 kutoka wilaya tofauti za mkoa wa Iringa lakini leo tumekuja na wahitaji 10 wa viungo vya miguu ambao wanakabidhiwa viungo hivi,”amesema Mgongo.
 
Kwa upande wao baadhi ya wahitaji waliopata viungo hivyo bandia wamemshukuru Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa, Ritta Kabati kwa msaada huo wakieleza kuwa utawasaidia kuishi na kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
 
Katika hatua nyingine, Ofisi ya Mbunge huyo imetoa shukurani kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa kwa kutoa ushirikiano wakutosha ikiwemo kuwasafirisha wahitaji hao kutoka Iringa hadi Dar es laam na kuwaomba wadau wengine mkoani humo kujitokeza kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu.
 
  • Video: Ufugaji mende unavyolipa
  • Chadema wamvaa Spika Ndugai kuhusu Tundu Lissu
  • Video: CAG kikaangoni, Zitto ageuka Mtikila

Lissu ajibu kauli ya Spika kuhusu kutokuwa na ruhusa, kuzurura
Israel yapiga ngome za Iran nchini Syria