Siku chache baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kueleza kuwa ameunda tume maalum ya kuchunguza taarifa za kifo cha Faru John katika hifadhi ya Sasakwa Grumet ikiwa ni pamoja na kuchunguza kaburi lake, imeelezwa kuwa faru huyo hakuzikwa.

Waziri Mkuu alitangaza hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na ripoti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyoeleza kuwa faru huyo aliugua na baadae kufariki akiacha watoto ambao wanaunda asilimia kubwa zaidi ya wanyama hao ndani ya hifadhi hiyo.

Mmoja kati ya wahifadhi aliyeomba jina lake lisitajwe, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa hakuna kaburi la faru huyo kwani kwa kawaida wanyama waliokufa bila kuwa na magonjwa ya mlipuko huachwa wawe chakula cha wanyama wengine.

“Faru John baada ya kufa aliondolewa pembe zake na kutupwa ili kiwe chakula cha wanyama wengine wanaotegemea mizoga, lakini kuna mifupa yake,” alisema.

Naye Mkurugenzi mkazi wa shirika la uhifadhi la Kimataifa la Frankfurt Zoological Society, Grald Bigurube aliungana na kauli ya mhifadhi huyo akieleza kuwa kwa kawaida wanyama wanaokufa hifadhini huwa hawazikwi.

Leicester City waipeleka kadi ya Vardy mbele ya FA
‘Tulidanganywa Ukeketaji umehalalishwa’