Makamu wa rais wa timu ya Simba, Geoffrey Nyange Kaburu amesema kuwa watani zao Yanga wanashangilia ubingwa hewa kwani ligi bado haijamalizika.

Amesema kuwa katika ligi yoyote duniani hakuna mtu anayeweza kutangaza ubingwa wakati mechi bado na kuna uwezekano wa timu yoyote kuuchukua ubingwa.

Aidha, Simba wanatakiwa kushinda zaidi ya mabao nane katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu huku wakiomba Yanga ifungwe zaidi ya mabao matano na Mbao FC mjini Mwanza ili wao wawe mabingwa.

Hali hiyo imeonekana kutowakatisha tamaa Simba na hawataki kusikia Yanga wakitangazwa kuwa mabingwa kabla ya mechi yao ya mwisho wao wakiwavaa Mwadui FC jijini Dar es Salaam.
“Sisi tunajua bingwa bado hajapatikana na tutaona hadi katika mechi ya mwisho. tutapambana hadi tone la mwisho.
“Hatuwezi kukata tamaa, huu ni mpira na vijana wako vizuri kabisa,” amesema Kaburu.

Hata hivyo, endapo mechi ya mwisho Yanga atakubali kufungwa atakuwa na pointi 68 sawa na Simba ambao viongozi bado wanaamini kuwa pointi tatu walizopokonywa dhidi ya Kagera Sugar zitarudishwa kwani wanataka kwenda FIFA kudai pointi zao na watakuwa na pointi 71.

Hali yazidi kuwa tete Kibiti, mwingine auawa kwa kupigwa risasi
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 18, 2017