Mlinda Lango wa Young Africans Ramadhan Kabwili amewaomba radhi, viongozi, mashabiki na wanachama kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame dhidi Nyasa Big Bullets, jana Jumapili (Agosti Mosi).

Kabwili alioneshwa kadi nyekundi dakika za mwisho za mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, kwa kuonesha mchezo usio wa kiungwana dhidi ya Mshambuliaji wa Nyasa Big Buletts.

Mlinda Lango huyo ambaye ni chaguo la tatu kwenye kikosi cha Young Africans ameomba radhi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuanfika: Nipende kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi uongozi wanachama, wapenzi na mashabiki wa @yangasc kwa tukio la kadi nyekundu lililotokea kwenye mchezo wetu wa leo (Jana).

Inaniuma sana, nilitegemea kuonyesha uwezo wangu kwenye mashindano haya nakuipambania team yangu.

Naona kama ndoto yangu imesimama na kuzima ghafla kwenye mashindano haya. Niwape matumaini wachezaji wenzangu kuendelea kuipambania team yetu na hatimae tuibuke kuwa washindi wa michuano hii.
#daima_mbele_nyuma_mwiko

Ratiba ya michezo ya leo Agosti 02/2021

UCHAMBUZI: Kocha Lwandamina hana la kujitetea
Biteko atoa siku 60 kufutwa leseni zisizofanya kazi