Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, Erasto Ngole amemkabidhi miche 500 ya Parachichi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Masimbwe inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi iliyopo katika eneo la Mkiu wilayani Ludewa.

Akikabidhi miche hiyo Ofisini kwake, Ngole amemueleza mkuu wa Shule ya Sekondari Masimbwe kuwa lengo la kutoa miche hiyo ya Parachichi ni kuiwezesha shule hiyo ya Chama cha Mapinduzi kumiliki mradi endelevu ambao baadaye utaifanya shule kusimama yenyewe ikiwa na uchumi mzuri.

“Nimeamua kutoa miche hii ya parachichi 500 ili baadaye iweze kuboresha uchumi wa shule yetu tuachane na tabia ya kuwategemea wadau, Parachichi hizi zikishaanza kuvunwa nakuhakikishia shule itakuwa na Uchumi mkubwa sana hilo litasaidia kukuza taaluma katika shule yetu, lakini naomba msiniangushe jamani nimetoa miche maeneo mengi lakini baadhi wameamua kuuza na kula pesa sasa Mwalimu naomba ukasimamie huu mradi”. amesema Ngole.

Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Masimbwe Mwalimu, Elyud Sanga amemshukuru Kiongozi huyo wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kwa kutoa miche hiyo bila malipo yeyote huku akiahidi kusimamia mradi huo waliouanzisha kikamilifu ili baadaye shule iweze kusimama yenyewe kiuchumi na kitaaluma.

Hata hivyo, Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe kupitia Idara ya wazazi inamiliki Shule mbili za Sekondari ambazo ni Masimbwe pamoja na Ludewa Sekondari zote zipo katika wilaya ya Ludewa Mkoani humo.

Video: Lissu asubiri muziki wangu - Ndugai, Adaiwa kumuua mdogo wake kisa mgawo kishika uchumba
Siasa zatajwa kukwamisha ujenzi wa kituo cha Afya