Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kumpongeza David Kafulila kwa kuibua sakata la la IPTL, Kafulila ameeleza kufurahishwa na kauli hiyo ya Rais Magufuli na kumpongeza kwa kuona utendaji wake huo.

Kafulila aliibua sakata hilo ambalo liliwahusisha vigogo kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo wanasiasa na viongozi kutoka Serikalini.

“Nimefurahishwa kuona mkuu wa nchi ameguswa na kutambua mchango wangu katika vita hii hatari ya ufisadi wa IPTL/Escrow kwakuwa imekuwa ikilitafuna taifa kwa muda mrefu sasa,”amesema Kafulila.

Aidha, amesema kuwa vita hiyo siyo ya kichama hivyo kila Mtanzania anatakiwa kuunga mkono ili kuweza kutokomeza na kuwakamata wale wote waliohusika na ufisadi huo ambao umeiliingizia taifa hasara kubwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa anatamani kuona hakuna jiwe lianlobaki katika ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ikwemo waliobeba mabilioni katika Lumbesa kutoka katika Benki ya Stanbic ambao hawajawahi kutajwa hadharani.

Video: Joh Makini ft Davido na 'kata leta'
Erdogan ajitosa kutatua mgogoro wa Qatar na nchi za Kiarabu