Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajia kuapishwa mapema hii leo ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka 7 ikiwa ni wiki mbili baada ya kuibuka mshindi kwa asilimia 98 katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki mbili zilizopita.

Sherehe za kula kiapo zitafanyika kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo wa Amahoro mjini Kigali, ambapo zaidi ya marais 20 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.

Aidha, Miongoni mwa marais wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Kagame ni pamoja na rais wa Sudan, Omar Al Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Hata hivyo, Uchaguzi huo ulikosolewa na baadhi ya mataifa kama Marekani ambayo ilisema hali ya siasa nchini Rwanda inatoa fursa kwa mtu mmoja pekee kuendelea kuiongoza nchi hiyo.

Lema ampigia magoti JPM, amtaka aruhusu maandamano
Museveni agonga mwamba kubadili Katiba