Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki ameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutekeleza kiukamilifi maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzannia, Dkt John Magufuli juu ya kupunguza kodi zisizokuwa za msingi.

Ameyasema hayo mara baada ya Rais Magufuli kuitaka TRA kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji ndani ya taasisi hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa.

“Niombe TRA maagizo haya ya Rais myatekeleze na sio kusema “tunayafanyia kazi”, private sector yetu inadidimia biashara nyingi zimefungwa na nyingine nyingi zimehamishiwa nchi jirani. sina uhakika hii inatafsiri gani katika makusanyo yenu.”amesema Kagasheki

Aidha, akizungumza na wakuu wa mikoa, mawaziri pamoja na wakuu wa mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, rais Magufuli amesema kuwa inathibitisha kuwa ufanisi kwenye ukusanyaji mapato nchini umepungua hivyo nchi haitakiwi kujilinganisha na nchi jirani.

Hata hivyo, rais Magufuli ametolea mfano wa kodi ya majengo kuwa ni kubwa sana, majengo yaliyosajiliwa mpaka sasa ni milioni 1.6 hivyo kuagiza kodi ya majengo iwe shilingi elfu 10 kwa nyumba ya kawaida, na shilingi 20 kwa nyumba za juu na shilingi elfu 50 kwa nyumba za mjini, zitozwe kulingana na hati ya kiwanja, na si idadi ya nyumba kwenye kiwanja.

Video: Serikali haitamvumilia kiongozi atakayekiuka maadili - Waziri Mkuu
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 11, 2018