Klabu ya Kagera Sugar imetangaza rasmi kuachana na Mlinda Lango kutoka Burkina Faso Nurdin Barola, baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja Mkataba.

Pande hizo mbili zimefikia makubaliano hayo, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, na imeamuliwa ni bora zikaachana kwa wema, ili kila mmoja aendelee na maisha yake ya soka.

Nurdin Barola alikua amebakisha Mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumiki Kagera Sugar, ambayo ilimsajili akitokea Namungo FC ya Lindi mwanzoni mwa msimu uliopita.

Kagera Sugar imetoa taarifa za kuachana na Mlinda Lango huyo ambaye pia aliwahi kuitumikia Biashara United Mara kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika: Thanks for Everything BAROLA ??.

Tunapemda kuwafahamisha kuwa, Kagera Sugar Football Club tumefikia makubaliano ya Kuvuja mkataba Uliosalia wa Mwaka mmoja 2022/2023 dhidi ya Mchezaji wetu Mlinda mlango NURDIN BAROLA ambaye alikuwa akihudumu Kama Mlinda mlango No.3.

Makubaliano haya yamefikiwa baina ya pande zote mbili na sisi Kama club tunamtakia kila la Kheri huko aendako.

Nurdin Barola alisaini mkataba wa Miaka miwili wa kukitumikia kikosi Cha Wanankurukumbi Hadi 2023.

Thanks for ll Everything BOROLA ???

Wengine walioachwa Kagera Sugar ni Peter Mwalianzi, Cosmas Lewis, Hassan Mwatelema, Nassoro Kapama, Mwaita Gereza, Erick Kyaruzi, Sadat Nanguo, Yusuph Mlipili na Jordan John.

Spika Tulia atoa somo mkutano wa Mabunge SADC
Azam FC kuweka kambi El Gouna-Misri