Wakazi wa mkoa Kagera wametakiwa kutobweteka kwa kutegemea misaada inayozidi kutolewa na mashirika mbalimbali na asasi za kiraia, kwani misaada hiyo imelenga kusaidia kujenga Miundo mbinu ya mkoa ambayo itakuwa inatoa huduma za kijamii na si kuwajengea nyumba kama walivyo jijengea fikra.

Hata hivyo wananchi wa Mkoa huo wametakiwa kutokusubiri kila kitu kutoka Serikalini kwani Serikali haina uwezo wa kumhudumia kila mmoja kulingana na mahitji yake, hivyo Serikali imejikita zaidi katika kutengeneza miundo mbinu ambayo itakuwa inatoa huduma kirahisi kwa jamii.

Mkoa wa kagera ulikumbwa na tetemeko la ardhi amabalo lilisababisha madhara makubwa kwa wananchi waishio katika Mkoa huo kwa kutokea vifo vya watu kadhaa.

 

Danny Drinkwater Kufungiwa Michezo Mitatu
Ndege yaanguka kwenye maegesho ya magari