Baada ya kuwepo kwa maneno mengi juu ya Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kutokucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs mwenyewe amefunguka.

Kagere hakucheza mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Hata hivyo Simba SC haikufuzu kutinga hatua ya nusu fainali kufuatia kichapo cha mabao 4-0 walichokipata Afrika Kusini kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Kagere amesema: “Ambalo lipo katika akili yangu ni kuhakikisha kila nikipewa nafasi ya kucheza nafanya vizuri kwa kutoa mchango kwa timu kupata kile ambacho tunahitaji.”

“Ndio maana ikitokea hata nimekaa nje bila kucheza huoni naonyesha tofauti yoyote ila ikitokea nimepewa nafasi ya kucheza tu huwa napenda kufanya mambo kama ambavyo yaliyotokea katika mechi ya Dodoma Jiji.

“Binafsi si mtu ambaye napenda kuongea zaidi bali natamani kufanya vitendo kama ambavyo kazi yangu inahitaji huwa nashukuru Mungu kila nikipata nafasi ya kucheza huwa hivyo,”

Sakata la kutocheza mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs lilimuibua wakala wa Mshambuliaji huyo na kudai hakufanyiwa uungwana kuachwa nje.

Mawaziri sekta ya Biashara EAC wakubaliana kuondoa vikwazo
Simba wamsimamisha Mkude