Kalamu ya @swalehmawele
Yanga anakwenda kucheza katika uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera Sugar sehemu ambayo huwa anapata matokeo mazuri mara kwa mara, mechi tano za mwisho ambazo Yanga amecheza Kaitaba ameshinda zote.

Pengine inakwenda kuwa mechi ngumu zaidi upande wa Kagera Sugar si kwa historia pekee bali hata kwa kukitazama ubora wa kikosi cha Yanga na hali ya kiakili waliyonayo hivi sasa.

Yanga wamepata ushindi mbele ya mtani wao na wanataka kuendeleza ushindi kwenye mechi za ligi kwa kuanzia leo.

Kila kitu kwa upande wa Kagera Sugar nakiweka mikononi mwa Francis Baraza, huyu ni aina ya kocha ambae anakuwa na mbinu sahihi katika mechi kubwa kinachomfelisha ni utekelezaji tu kwa wachezaji katika hizo mbinu husika.

Msimu uliopita alifanikiwa kuibadilisha Kagera Sugar kwa kiasi kikubwa na ikawa timu inayopata matokeo mazuri, anaweza akampa mechi ngumu Mohammed Nabi lakini swali litabaki ni vipi wachezaji wake watahimili presha dhidi ya qualify ile ya Yanga hivi sasa.

Francis Baraza ni muumini wa 3-5-2 na Mohammed Nabi ni muumini wa 4-2-3-1, inaweza kuwa wachezaji watatu dhidi ya mmoja katika safu ya ushambuliaji ya Yanga na ikawa wawili dhidi ya wanne katika safu ya ushambuliaji ya Kagera Sugar.

Hapa itabaki kuwa nani anaweza kucheza katika madhaifu ya mpinzani wake na kuutumia ubora wake kumuadhibu, binafsi sijaiona Kagera Sugar katika mechi yeyote msimu huu na kuanzia hapa natagemea kuona taswira ya Baraza baada ya kuiandaa timu kuanzia mwanzoni mwa msimu.

Diara afichua siri ya ubora wake
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 29, 2021