Shirikisho la Soka la Morocco ‘RMFF’ limeelezea sababu za kutoiruhusu timu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini kuingia nchini humo kwa mchezo wa kwanza wa ‘Kundi C’ wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad Athletic.

Tangu juzi taarifa zinaeleza kuwa Kaizer Chiefs wamenyimwa kibali ‘VISA’ cha kuingia nchini Morocco licha ya kuwa tayari wamethibitisha (Booking) maandalizi ya safari ya ndege na Hoteli watakapokua nchini humo.

‘Amakhosi’ wanatarajia kucheza mchezo huo keshokuta Jumamosi (Februari 14) mjini Casablanca, lakini mpaka sasa Shirikisho al soka Barani Afrika CAF halijatoa taarifa yoyote kuhusu mkanganyiko huo.

Miamba hiyo ya Soweto ilitarajiwa kuondoka Afrika Kusini jana Jumatano usiku lakini ililazimika kuahirisha safari,  huku akitarajia huenda leo wakapata jibu sahihi kutoka CAF na mamlaka za Morocco.

“Shirikisho la Soka  Morocco lilituma barua kwa Kamati ya Vilabu ya CAF kuifahamisha kuwa mamlaka ya Morocco waliamua kutoruhusu mchezo wa Wydad Casablanca na timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini utakayofanyika Februari 13 huko Casablanca kwa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, kwa sababu ya afya na usalama inayohusiana na maendeleo ya hivi karibuni ya Covid-19, “ilisomeka taarifa kutoka RMFF.

Shirikisho la Soka la Morocco lilitaka Shirikisho la Soka Barani Afrika kuahirisha mchezo huo, au kuibakiza tarehe hiyo na kufanyika katika nchi nyingine ikiwa jibu lao halitakubaliwa.

Mwamnyeto safi, Ntibazonkiza atuma ujumbe
Ndugulile: TPC ongezeni matumizi ya TEHAMA kuhudumia wateja