Mwigizaji mahiri kutoka katika tasnia ya Bongo Movie Frida Kajala, hatimaye amerusha jiwe gizani kufuatia muendelezo wa machapisho kadhaa ya aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki Harmonize akimtaka warudiane na kusahau yaliyopita.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Kajala ameonekana kutumia maneno yanayoshabihiana na majibu ya mfululizo wa  maombi ya msanii Harmonize.

Mwigizaji huyo amegusia kuhusu watu ambao wanamsisimko wa muda wote kurejea kwenye maisha yako, ili kurudi kukujaribu au hata kukukosea zaidi.

Jumbe hizo kadhaa za Kajala zimetafsiriwa kama kijembe kwa Harmonize ambaye kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili sasa, mwimbaji huyo amekuwa akiomba msamaha ili ikiwezekana wawili hao warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa awali.

“Usiwe yeyote wakati mwingine, Kwanza jua thamani yako, pili jua namna ya kuendesha mihemko yako, Tatu kamwe usihangaike.

Usijihusishe, kumbuka kilichotokea wakati uliopita, huwezi kumbadilisha kila mtu, endelea na maisha yako, usimuache yeyote akuchezee, hatakama unawapenda.

Ni rahisi kumpata mtu mwingine mpya,  lakini ni ngumu kumpata mkweli” Unasomeka muendelezo wa machapisho kadhaa ya Kajala.

Hivi karibuni Konde boy alishika nafasi kwenye vichwa vya habari mbali mbali kupitia njia aliyoamua kuitumia kujaribu kumuomba radhi ili kumrudisha Kajala kwenye maisha yake.

Konde alianza kwa kubandika bango kubwa la matangazo lenye picha yake na mwigizaji huyo huku ikidaiwa kuwa alilipia zaidi ya Milioni 12, ili kujaribu kudhihirisha upendo kwa hadhira kwa dhana ya kuwa pengine angeweza kumrudisha mrembo huyo lakini bado alipuuzwa.

Mara ya pili aliomba radhi hadharani kupitia kwenye mahojiano maalumu aliyofanya na kituo cha runinga cha Tv E akiwahusisha Kajala na binti yake Paula lakini bado haikuzaa matunda ya kusudio lake kutoka na ukimya uliodumishwa na Kajala.

Harmonize a.k.a Tembo mmiliki wa Hit song ‘Never give up’ ameendelea kudhihirisha kuwa si mkataji tamaa kwa urahisi, baada ya yote hayo, bado ameweka wazi kununua magari mawili kwa ajili aina ya Range Rover kwa ajili ya mrembo huyo.

Ahmed Ally arudisha majibu Young Africans
Mwafulango: Simba SC, Young Africans zikamia sana