Muigizaji maarufu nchini Frida Kajala maarufu Kajala amemzawadia binti yake Paula, gari aina ya Toyota Crown mpya, hii ni punde mara baada ya kuachana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Paula ameweka wazi kuwa alitarajia kupata zawadi lakini si nzuri na kubwa kama aliyopatiwa na mama yake.

“Nilijua 2023 itakuwa nzuri lakini sikujua inaweza kuwa nzuri hivi. Kuna akina mama na kuna mama yangu, siwezi kufikiria maisha yangu bila wewe, Asante Kajala Fridah,” Paula aliandika.

Kajala akimkabithi Paula Gari. photo: Instagram

Hivi karibuni Kajala na Harmonize wawili hao waliachana katika mazingira yasiyoeleweka kutokana na kuwa sababu za wawili hao kutengana kutowekwa hadharani.

Itakumbukwa kuwa Raymond Shaban Mwakyusa maarufu (Rayvanny) alithibitisha kuachana na Paula mwaka Septemba, 2022 katika onesho lake huko Sumbawanga.

Rayvanny na Paula enzi za uhusiano wao. Picha: Paula/Instagram

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “Usiruhusu mapenzi yakuchanganye, usifananishe mapenzi na chakula, nilihitaji amani ya moyo wangu na kukatisha uhusiano wangu na Paula,”

Also read: Mtoto wa Lil Wayne acharuka baba yake kushindanishwa na wasanii wachanga

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 9, 2023
Bei mpya ya vifurushi kutangazwa