Muigizaji wa Filamu za Kibongo Tanzania, Kajala Masanja aamua kujibu mapigo dhidi ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifuatilia maisha yake na kumzushia mambo yasiyofaa binti yake Paula.

Ambapo video ya binti asemakaye kuwa ni bintiye Kajala, Paula zisizo na maadili zilirushwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu ambao wanachuki na Kajala ikiwa kama kumdhalilisha kajala na mwanae.

Wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ilirushwa video iliyosemekana, Paula bintiye Kajala ikiwa ikionesha anafanya mapenzi na mtu mzima ndani ya gari.

Paula ni mtoto mwenye miaka chini 18, pia ni mwanafunzi hivyo kama mama mzazi wa mtoto huyo hakufurahishwa na kitendo cha uzushi huo kwani alithibitisha video iliyokuwa ikiendelea kusambaa mitandaoni, binti aliyetumika kwenye video hiyo sio binti Kajala, Paula.

Hivyo kupitia mtandao wa kijamii kajala alaiandika haya.

”Jamani sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile” kwa sababu najua binadamu kuongea mmezoea.

”Ila katika kuongea kwenu, kuingilia na kujudge my life naomba msimuingize mtoto wangu. sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja” nimeona kuna video inasambaa mnasema ni mwanangu na mnajaua kabisa sie Paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu.”

Ameongezea ”Nilinyamaza ” ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya, mnahisi yeye hana moyo ? au mnahisi haumii ? Mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi ” Vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe, fanyeni tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha”.

 

UVCCM: bila CCM Tanzania isingekuwa na Demokrasia huru
Video: Possi - Nitajiuzulu ubunge, Mjadala kupanguliwa mawaziri washika kasi