Ruvuma, Jeshi la Polisi linamshikilia Mohamed Luambano (70) mkazi wa Mtelamwai wilayani Namtumbo kwa tuhuma za kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani na kiganja cha mkono wa kulia mdogo wake, Abeid Luambano (65) na hatimaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema lilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika kitongoji cha Doroba, kijiji cha Mtelemwa baada ya mwili wa marehemu kukutwa nyumbani kwake.

Maigwa amesema, Abeid kabla ya kuuawa, alivamiwa ghafla na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kisha kutolewa nje ya nyumba yake na kuanza kupigwa na kitu chenye ncha kali hadi kupoteza maisha.

Kutokana na tukio hilo kaka wa marehemu, amekamatwa kwa mahojiano zaidi kutokana na madai kwamba siku za karibuni kumekuwapo na kutoelewana kati ya ndugu hao.

Aidha inasemakana kwamba ugomvu huo ulisababishwa na Abeid kuchomewa nyumba yake aliyokuwa akiishi akimtuhumu kaka yake na mtoto wake aliyetajwa kwa jina la Msajiri kuwa walikuwa wakimfanyia vitu vibaya.

Mtoto huyo wa Luambano amekimbia na kutokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo la mauaji.

Kamanda maigwa ameendelea kuelezea kwamba juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.

Ajinyonga chumbani kwake kisa madeni ya vikoba
Kapt. Mkuchika kumwakilisha Rais Magufuli sherehe za kuapishwa Mfalme Japan