Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Kala Jelemiah amejipanga kuweza kuilipa heshima aliyopewa baada ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu kumsifia Kala kwa utunzi bora wa wimbo wake wa ‘kijana’.

Kala Jeremiah amesema kuwa amefanya muziki kwa muda mrefu lakini hajawahi kupata pongezi kwa kazi ambazo amesha wahi kuzifanya kama ilivyo tokea kwa Makamu wa Rais Mama Samia kumpongeza kwa kazi yake ya Kijana ambayo inafanya vizuri kwa sasa.

“Nimefanya muziki kwa mda mrefu ila sijawahi kupata pongezi kutoka kwa kiongozi mkubwa wa nchi kama yule tena mbele za maelfu ya watu mara nyingi tumekuwa tukikutana na viongozi wa kawaida na kutupa pongezi za kawaida” Amesema Kala.

Baada ya msanii wa Hip Hop Kala Jelemiah kula shavu la nguvu la kusifiwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa ngoma yake mpya aliyoachia hivi karibuni “Kijana” ni nzuri, amesema anajipanga kuilipa heshima hiyo aliyopewa na kiongozi wa nchi.

Hata hivyo, Kala ameongeza kuwa alizipokea salamu za Makamu wa Rais kutoka kwa watu wengi  kitendo ambacho amekipokea kwa mikono miwili na kuwa kauli hiyo ya Makamu wa Rais imempa deni la kuendelea kukaza buti na kuandaa nyimbo  nyingi  zitakazo kuwa mkombozi kwa Jamii.

Mrithi wa Mugabe aanza kusaka ‘huruma’ ya Magharibi

Comments

comments