Msanii wa muziki wa Hip pop Kala Jemiah amedai kuwa amefanya tafiti ndogo juu ya muziki wa sasa na mashabiki wake  na kugundua kuwa kiki ni kitu muhimu sana katika muziki wa sasa ili kukuza jina na muziki unaofanya, bila kutafuta kiki au kufanya kitu ambacho mashabiki wako watakuongelea muda wote inapelekea kusahaulika kimuziki.

Kala Jeremiah alizungumza kwa upande wake hawezi kutafuta kiki kwani anaamini ameshazeeka, majukumu ya kifamilia yameongezeka na kuna baadhi ya vitu ambavyo amezungumza kuaachana navyo kwani tayari ana mtoto.

Hali hii ni tofauti na muziki wa zamani, miaka ile msanii alikuwa anajulikana kupitia muziki wake au albamu yake aliyoifanya.

”Muziki wa sasa umebadilika kutokana na mashabiki kutaka vitu fulani ambavyo sio vya kawaida,” amesema Kala Jeremiah.

Katika tafiti ndogo aliyoifanya amegundua jina la rapa, Harmorapa ni kubwa kuliko hata majina ya baadhi ya wasanii wa muziki huo ambao tayari wana albamu mbili sokoni.

”Mimi hivi karibuni nilikuwa na msichana mmoja nikataka kujua nguvu za baadhi ya wasanii wa hip pop, nikawa namuuliza kuhusu wasanii watano ambao wengine wana albamu zaidi ya mbili sokoni alisema hawajui, lakini nilipomuuliza kuhusu kumjua Harmorapa alijibu kuwa huyo namjua sana, tena ana wimbo mmoja,” amesema Kala Jeremiah.

Ameongeza kwa kusema, ”kwaiyo nikagundua huu mziki sasa hivi msanii anatakiwa kuzungumziwa kila mara, sio ukitoa tu ngoma basi, kuna namna ambavyo unaweza kufanya ili uendelee kuwa midomoni kwa mashabiki”.

Ukifanya tafakari ndogo juu ya tafiti na mtazamo wa mwana Hip pop Kala Jeremiah, utagundua kuna ukweli ndani yake siku hizi watu wanatafuta njia ya kutokea kimuziki kwa kutafuta visa ili wajadiliwe mitandaoni na katika vyombo vya habari.

Ni jambo zuri na jema kutengeneza jina mtaani kwanza kisha  kuzama katika mziki maana tayari utakuwa unajulikana kwa kitu fulani ambapo ukiingia kwenye muziki ni rahisi watu kutaka kuujua muziki wako zaidi kama ilivyo kwa Harmorapa, Luludiva na Mimi Mars, ambao ni chipukizi lakini muziki wao unafanya vizuri sokoni.

Mbowe na Mkewe wabanwa tena, TRA yawaburuza Mahakamani
Kala Jeremiah: Jina Harmorapa ni kubwa kuliko baadhi ya majina ya wasanii wenye albamu mbili sokoni