Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa muda wa siku tano kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kuhakikisha linafanya matengenezo ya mtambo wa kufua umeme ili kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika baadhi ya maeneo nchini.

Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo mkoani Dar es salaam wakati wa ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme cha SONGAS.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt Titto Mwinuka amemuhakikishia Dkt. Kalemani kuwa watasimamia matengenezo ya mtambo huo na kumaliza tatizo hilo la kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo nchini.

WHO: Hakuna dalili za corona kumalizika mwaka huu
Waziri Mpango arejea kazini