Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alilazimika kukataa ofa ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka England na klabu ya Liverpool Daniel Sturridge saa chache kabla ya dirisha halijafungwa usiku wa kuamkia hii leo.

Saa kadhaa kabla ya harakati za usajili kusitishwa huko barani Ulaya, tovuti ya Goal iliripoti uwezekano wa klabu ya Arsenal kumsajili kwa mkopo Sturridge akitokea Anfield, lakini nia ya Wenger haikuwa hivyo.

Babu huyo kutoka nchini Ufaransa, alionyesha kuwa tayari kufanya biashara na Liverpool ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini upande wa majogoo wa jiji waligoma kufanya hivyo hadi muda wa uhamisho ulipofikia tamati.

Mzozo baina ya pande hizo mbili uliripotiwa na tovuti ya The Sun na muda ulivyokua unayoyoma ikabadilisha upepo na kutoa taarifa za uwezekano wa Sturridge kusajiliwa kwa mkopo, lakini bado mambo yalikwenda mrama.

Hata hivyo wakati Wenger anapingana na Liverpool, alikua anafahamu ana hazina ya kutosha ya wachezaji wanaocheza nafasi ya ushambuliaji, kutokana na kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania Lucas Perez huku Danny Welbeck akiwa njiani kurejea uwanjani mwishoni mwa mwaka huu.

Sturridge amekua na wakati mgumu wa kutimiza malengo ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool tangu mwanzoni mwa msimu huu, na aliamini kuondoka kwake Anfield huenda kungempa nafasi kutimiza azma ya kuepuka janga hilo.

Kweli Ng'ombe Wa Masikini Hazai, Shkodran Mustafi Aumia
The Three Lions Yapata Mtihani, Foster Aondoka Kambini