Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amewaonya watu wanaopanga kushiriki maandamano ya Aprili 26 yanayohamashishwa mitandaoni kutojaribu kwani hawatabaki salama.

Amesema kuwa watu watakaoshiriki watajikuta katika matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na ukilema.

Aidha, Kamanda Muroto amewaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuitumia kwa faida ya taifa kuhamasisha maendeleo.

“Watakaoingia barabarani siku hiyo watapata matatizo makubwa kwani wengine watajikuta wakiwa vilema. Hivyo, ni vyema kuitumia mitandao katika kuhamasisha maendeleo badala ya kuhamasisha mambo ya kijinga,” alisema Muroto alipozungumza na waandishi wa habari juzi.

Jeshi hilo limewakamata watu wawili ambao ni dereva wa Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF), Amandus Manchali na Yuda Mbata ambaye ni mkulima mkaazi wa Bahi.

Kamanda Muroto aliwafananisha watu wanaoandaa maandamano hayo kama watu walioshiba na kuvimbewa ambao wamesahau nchi ilipotoka ambao wanaweza kuhamishia choo ndani ya nyumba zao.

Mamba avamia hospitali, ahusishwa na ushirikina
Maneno ya busara Machi 23, 2018