Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amemaliza muda wake wa kulitumikia jeshi la polisi na leo itakuwa siku yake ya kustaafu rasmi.

Kamanda Kova amethibitisha taarifa za kustaafu kwake alipokuwa anaongea na kipindi cha Kumekucha cha ITV, mapema leo asubuhi.

“Ninyi mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi,” Kova anakaririwa.

Akizungumzia kazi aliyoifanya, Kova alieleza kuwa alijitahidi kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya kihalifu jijini Dar es Salaam.

Kova alihamishiwa katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam mwaka 2008 akitokea jijini Mbeya.

Majogoo Wa Jiji Wajikongoja Taratibu
Baby Madaha aanguka Chooni