Basi la abiria la Allys linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza, leo limeteketea kwa moto likiwa katika eneo la Bahi Mkoani Dodoma.

Dar24 Media imezungumza na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Gilles Muroto ambaye ameeleza chanzo cha ajali hiyo.

“Ni ajali ya kawaida, ni hitlilafu, chanzo kupasuka kwa booster ya upande wa kushoto zilizopelekea mbanano wa break na kutoa cheche zilizopelekea gari kuwaka moto,” Kamanda Muroto ameiambia Dar24 Media.

Akizungumzia madhara yaliyotokea, amesema kuwa hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwakuwa abiria wote wako salama.

Moto wateketeza mabweni shule ya African Muslim

Mwinyi ataja sababu za kugombea urais Zanzibar

Wabunge washtukia pesa za Covid-19 kupigwa, watoa siku 60
Rwanda yamsaka ‘mpelelezi wake’ kwa tuhuma za mauaji ya kimbari