Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemshikilia Rajab Ramadhan [32] aliejifanya askari polisi Kwa kutapeli watu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma Kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema kuwa kwa muda Mrefu kijana huyo anayeishi eneo la Area A jijini humo amekuwa akijipatia huduma mbalimbali kwa udanganyifu akijifanya askari polisi na kutishia watu kwa silaha bandia.

Kamanda Muroto ametaja vifaa alivyokuwa navyo mhalifu huyo kuwa ni sare ya polisi Jangle Green, pistol ya bandia na hoster yake, picha akiwa na sare za jeshi [JWTZ] huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa kijana huyo alishawahi kuhudhuria mafunzo ya JKT na Kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu.

Aidha, katika hatua nyingine Kamanda Muroto amesema kuwa jeshi hilo limekamata vifaa vya NIDA ambavyo ni kamera 12 ambapo mtumishi wa NIDA Ezekiel Subugo [24] aliiba vifaa hivyo ofisini na kuwauzia watu mitaani na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Pia Jeshi hilo limemkamata Musa Pungu akiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kiasi cha kete 132 zilizofungashwa katika vinailoni ambapo Kamanda Muroto amesema kijana Musa ameharibu vijana wengi kwa madawa ya kulevya katika Mtaa wa Hazina jijini Dodoma hivyo mtuhumiwa na wenzake wanne watafikishwa mahakamani.

Sanjari na hayo, Kamanda Muroto ameipongeza Kampuni ya INNOMAX kwa kulikabidhi jeshi hilo pikipiki mbili mpya aina ya HAOJUE na HONGLOG zenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni 4 Kwa ajili ya kufanyia doria huku akiwaasa Watanzania wengine kuwa na uzalendo wa kusaidia jeshi hilo.

Raia watano wakigeni wanaohusishwa kumteka Mo Dewji kukamatwa
Video: "Sijamsaini Q Chief, nimemsaidia gari" - Harmonize