Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro jana alithibitisha nia ya Jeshi hilo ya kumkamata Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kamanda Siro alisema kuwa Jeshi hilo lilimpiga marufuku Zitto kufanya mikutano ikiwemo kongamano hilo kwani nia yake ni kufanya uchochezi lakini alikiuka maagizo hayo.

“Zitto tulimkataza asifanye mkutano wowote na leo (jana) tutampata na tutamkamata tu, na huo mkutano anaotaka kufanya ofisini kwake ni marufuku kwa sababu lengo lake ni uchochezi,” kamanda Siro alimwambia mwandishi wa gazeti la Mtanzania.

Kamanda Sirro alieleza kuwa lengo la Jeshi hilo ni kuhakikisha kuna amani nchini kwani bila amani watu hawatafanya siasa. Aliwataka wanasiasa kutii sheria.

“Kwa kawaida polisi tunatoa ulinzi, kwa hili hatutampa nafasi mtu anayeichafua nchi,” alisema Kamanda Sirro.

Jana, Zitto alijitokeza mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya chama chake kueleza kuwa hakifahamu alipo na kwamba amekuwa akiviziwa na Polisi kwa lengo la kumkamata.

Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamisi, ilisema kuwa baada ya mkutano huo na waandishi wa habari, Zitto alipigiwa simu na Jeshi la Polisi na kutakiwa kufika katika Kituo Kikuu cha Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Zitto aliitikia wito na kuhojiwa kwa saa moja akiwa na wanasheria wake, kisha kuachiwa.

Video: 'Wapinzani hatuzingatii Sheria wala Katiba, tunavuruga chaguzi' - Augustino Mrema
Everton Wamalizana Na Ronald Koeman