Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro ametoa taarifa kuhusu tukio la majambazi kuvamia na kuua askari polisi wanne waliokuwa wakilinda tawi la Benki ya CRDB lililoko MBande, wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kamanda Sirro amesema kuwa taarifa za awali za uchunguzi zimeonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na kwamba walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana zamu ya lindo, ndipo walipowavamia ghafla na kuwafyatulia risasi.

Akizungumza na Radio One, Kamanda huyo amesema kuwa wahalifu hao walivamia pia kituo cha polisi na kuvunja stoo kisha kuchukua sare za jeshi la polisi pamoja na silaha. Amesema gari la polisi lilikuwa katika eneo hilo lilichakazwa kwa risasi.

Gari la Polisi lililokuwa na askari

Gari la Polisi lililokuwa na askari

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” alisema Kamanda Siro.

Kwamujibu wa Kamanda Siro, askari mmoja aliyekuwa lindo katika eneo hilo alifanikiwa kuwatoroka majambazi hao na ndiye aliyetoa taarifa ya kilichojili.

Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa operesheni ya kukomesha majambazi ambayo ilifanikiwa na kusababisha baadhi yao kukimbilia nchi za jirani, waliosalia wameanza kujikusanya na kufanya matukio ya kihalifu.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Siro amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya watu watakaojitambulisha kuwa wao ni askari bila kuwaonesha vitambulisho vyao.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akimjulia hali askari aliyejeruhiwa

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akimjulia hali askari aliyejeruhiwa

Video: Jengo kubwa la hosptali lenye thamani ya bilioni 8.8 kujengwa Dar
Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars, Awatema Ulimwengu, Juma Abdul