Maafisa waandamizi wa mashirika ya upelelezi nchini Marekani wako katika kikao cha mahojiano kwa ajili ya tathmini ya  vyombo vyao kwamba Urusi ilifanya udukuzi katika uchaguzi wa rais na kumsaidia Donald Trump kushinda.

Kikao cha mahojiano  cha  kamati  ya huduma  za  majeshi  ya  taifa kuhusu  kitisho mtandaoni  leo Alhamis  kimekuja  siku  moja  kabla ya  rais  mteule  wa  Marekani Donald Trump  kupewa taarifa  na  wakurugenzi  wa  mashirika  ya  ujasusi  CIA  na  lile  la uchunguzi  wa  makosa  ya  jinai FBI, pamoja  na  mkurugenzi wa usalama  wa  taifa, kuhusiana  na  uchunguzi  juu  ya  madai  ya udukuzi.

Lakini msemaji  wa  Ikulu  ya  Marekani  ya  White House, Josh Earnest  amesema tathmini  iliyotolewa  kwa  pamoja  na  vyombo vya  upelelezi inaonesha  wazi  kuwa Urusi  ilikuwa  ikiingilia  shughuli za  uchaguzi  nchini  Marekani.

Tarifa hiyo ambayo  ilitolewa  na  vyombo  vya  upelelezi Oktoba mwaka  2016  kabla  ya  uchaguzi inaweka  wazi kwamba  Urusi ilikuwa  inaingilia  kati  katika  uchaguzi  woete na kuwalikisha mtazamo  wa  pamoja  wa  mashirika  17 tofauti  ya  upelelezi. Hii  si kawaida  ya vyombo  hivi  kufanya  kazi. Hali  ya mawazo yanayolingana, hususan hali  ikiwa  ya  mvutano, ni  suala la kutafakari. Uamuzi  wa  vyombo  vya  upelelezi, sio tu  kufikia hitimisho  lakini kuiweka  wazi ripoti  yao, ni  jambo  kubwa  na nafikiri inaakisi kina cha hali  yao  ya  kuamini tathmini  yao.”

Shutuma  za  Urusi  kuingilia  katika  uchaguzi  wa  mwaka  2016 kwa kudukua kurasa  za  barua  pepe  za  chama  cha  Democratic kilipelekea Rais Barack Obama  alilipize  kwa kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi  mwishoni  mwa  mwezi Desemba  kwa  kuchukua  hatua  ya  kuweka  vikwazo vinavyolenga mashirika  ya  ujasusi  ya  Urusi, lile  la  GRU  na  FSB, ambayo Marekani  ilisema  yanahusika.  GRU ni  shirika  la  Urusi linaloshughulika  na  masuala  ya  ujasusi  wa  kijeshi. Lile  la FSB ni mrithi  wa  shirika  la  wakati  wa  enzi  za  Umoja  wa  Kisovieti  la KGB.

Makamba afanya uteuzi wa wajumbe bodi ya NETFUND
Trump kuifuta sheria ya afya Obamacare