Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kesho Jumamosi Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13.
Malalamiko hayo ni:
- Mchezaji Ametre Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa pamoja na kufikia mafaka.
- Klabu ya Coastal Union dhidi ya Simba kuhusu madai ya fidia kwa wachezaji Hamad Juma na Abdi Banda.
- Ally Rashid Ally dhidi ya Simba, malalamiko ya kunyimwa stahiki zake
- Mchezaji Abdallah Juma dhidi ya Mbeya City, madai ya malimbikizo ya mshahara, fedha za usajili na gharama za matibabu.
- Simba dhidi ya Young Africans, madai ni kuingia mkataba na mchezaji Hassan Kessy wakati ana mkataba na Klabu ya Simba
- Kocha Abdul H. Banyai, kesi ni madai ya stahiki zake.
- Coastal dhidi ya Young Africans, madai ya fidia ya matunzo ya mchezaji Juma Mahadhi
- Saleh Malande dhidi ya Ndanda FC madai ya uvunjikaji wa mkataba
- Coastal Union dhidi ya Mbeya City, madai ya fidia ya fidia kwa matunzo ya mchaji wao.
- Sputanza FC dhidi ya Mbeya City, madai ya ada na usajili na mishahara
- Kimondo FC dhidi ya Ruvu JKT, majibu ya kumalizana kati ya timu hizo mbili
- Mathias Lule dhidi ya Stand United, taarifa ya kushindwa kufikia makubaliano ya kulipana.
- Kimara United FC dhidi ya Kurugenzi FC, pingamizi la mchezaji Martine Sepeni kusajili timu ya Kurugenzi ya Iringa.