Katika kuhakikisha inafikia malengo yaliokusudiwa, Kamati ya marekebisho na kuandika upya katiba ya ZFA imefanya makadirio ya Bajeti ya matumizi ambayo yatafanikisha kufanya marekebisho na kuandika upya katiba iliopendekezwa, bajeti hiyo jumla ni shs Milioni thalasini na tisa , laki nane na hamsini elfu (39,850,000/=).

Bajeti hiyo imejumuisha gharama zote ambazo zitatumika katika zoezi hilo ikiwemo usafiri , posho la vikao, posho la kukimu maisha na baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika zoezi hilo.

Katiba hiyo iliopendekezwa inatakiwa lazima ikidhi vigezo na masharti yanayokwenda sambamba na matakwa ya makubaliano yaliofanyika Mahakama kuu tarehe 26/11/2015 na kufuata misingi madhubuti ya FIFA, CAF, CECAFA na TFF katika kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu ndani na nje ya Zanzibar.

Kamati hiyo inatarajia kuanza kuzitembelea Wilaya kuanzia tarehe 20/05/2016 ambapo ZFA itakuwa tayari imeshawasilisha Fedha za matumizi yanayohitajika.

Viongozi sita (6) waliochaguliwa kwenye kamati hiyo ni Afan Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali Hamad (Msaidizi Katibu), pia yumo Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Wanawake (Twiga Stars) Nassra Juma na wengine ni Eliud Peter Mvella na Ame Abdallah  Dunia.

Gebermedhin Haile kukaimu Nafasi Ya Yohannes Sahle
Majina ya vigogo 45 wenye akaunti nono nje yaanikwa