Kamati ya utendaji ya Young Africans imeendelea kufanyia marekebisho nafasi mbalimbali na leo imetangaza kuvunja Kamati ya Mashindano.

Kamati ya Mashindano Young Africans ilikuwa chini ya Mwenyekiti, Rodgers Gumbo, Makamu wake, Saad Mkhiji na wajumbe ni Hamad  Islam, Makaga, Leonard Bugomola, Ally Kamtande, Said Side, Bonnah Kamoli, Sudi Mlinda, Tom Lukuvi, Martin Mwampashi, Hamza Jabir Mahoka, Edward Urio, Kawina Konde, Abednego Ainea na Edwin Muhagama.

Hatua hiyo inakuja siku mbili baada ya klabu kuvunja benchi zima la Ufundi liliokuwa chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, ambaye nafasi yake imekuchuliwa na Charles Boniface Mkwasa ‘Master’.

Ni dhahir maamuzi haya ya kamati ya utendaji ya yanafuatia baada ya timu ya Young Africans kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kufuatia kuchapwa 3-0 na wenyeji, Pyramids FC Jumapili Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo.

Matokeo yaliifanya Young Africans kutolewe kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Mwanza wiki mbili zilizopita.

Simba yashindwa kuunguruma Dar es salaam
Mbunge aponda mvuto wa wahudumu ndege za ATCL

Comments

comments