Spika Job Ndugai ametoa agizo kwa kamati ya Bunge Wizara ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mwenyekiti Mussa Azan Zungu kufanya uchunguzi kuhusu sakata la mwanamke, Amina Rafael aliyejifungua katika kituo cha Polisi cha Mang’ula wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Ambapo mwanamke huyo alikamatwa badala ya mume wake aliyekuwa akisakwa na polisi kwa tuhuma za kununua kitanda cha wizi na kuwekwa mahabusu kwa saa 10.

Hata hivyo mwanamke huyo amesema alipopata uchungu alitoa taarifa polisi lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na kuamua kutoka nje ya ofisi hiyo na kukaa kwenye majani na kujifungulia hapo.

Serikali imelipokea jambo hilo kwa uzito na tayari Wizara husika imeahidi kuchunguza tukio hilo lililowakilishwa Bungeni na Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ambaye katika kuomba mwongozo huo ameonesha kutiwa shaka na uchunguzi huo unaotarajiwa kufanyika akidai kuwa pamoja na kuwa Naibu Waziri Masauni kukiri kutokea kwa tukio hilo RPC alikana kutokea kwa tukio hilo mkoani kwake.

Hivyo Lijualikali amependekeza wakati uchunguzi unafanyika mwanamke huyo aweze kuitwa na kamati hiyo ili ahojiwe na kusema ukweli.

 

 

 

 

Video: FID Q ametangaza rasmi mambo haya mawili,"Watakutana na madude mapya"
Mohamed Salah aiweka njia panda The Pharaohs

Comments

comments