Kamati ya Dk Harisson Mwakyembe iliyokuwa ikitafuta chanzo cha kufeli wanafunzi wengi katika mitihani ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (LST), imependekeza kuanzishwa kwa mtihani maalumu wa kuingia LST.

Dkt. Mwakyembe amesema wakati akikabidhi ripoti ya kamati, baada ya kusikiliza maoni ya wadau 141 kamati imeona ni muda muafaka wa kufufua Baraza la Elimu ya Sheria (CLE), iliyo na mamlaka ya kusimamia taaluma za sheria nchini.

Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kamati Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro. Picha ya Michael Matemanga.

Amesema, “Serikali iliundie sekretarieti, kuipa bajeti na ofisi yake, ili litekeleza majukumu yake na suala hili halina budi kutekelezwa, ili CLE ianze kazi mapema iwezekanavyo.”

Kamati hiyo, iliundwa Oktoba 12, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro baada ya idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo LST, ambapo wadau walitoa maoni tofauti kuhusiana na suala hilo.

Uganda 'yacopy' na 'kupaste' kwa Wakenya
Matumaini mapya uokoaji tetemeko la ardhi