Kambi iliyokuwa ikihifadhi na kutumikisha watoto kutoka mikoa mbalimbali imeteketezwa kwa moto, pia mmiliki wa kambi hiyo Ustaadhi Saad Suleymani amekamatwa akituhumiwa kulaghai na kutumikisha watoto.

Zoezi hilo limefanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama  wilayani Hanang Mkoani Manyara, ambapo mmiliki wa kambi hiyo alikuwa akiitumia kulaghai na kuwatumikisha watoto katika shughuli za ufugaji na kilimo katika eneo la pori la kijiji cha Diloda.

Akizungumzia hatua ya kuiteketeza kambi hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sarah Ali Msafiri amesema kamati yake imebaini kuwepo kwa kambi hiyo kufuatia kufa maji kwa wanafunzi wawili kwenye rambo la kambi hiyo Machi 3 mwaka huu na kumgundua mmiliki huyo ambaye amekiri kuwatumikisha watoto kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara na Dodoma kwa kutumia mwamvuli wa Madrasatul Al Badil ili kujinufaisha, lakini pia kamati hiyo ikieleza kukosa vielelezo halali vya umilikishwaji wa ekari 63 za eneo hilo vilivyotolewa na Serikali ya kijiji hicho.

Nae Mmiliki wa kambi hiyo Ustaadhi Saad Suleyman akizungumza kabla ya kuangua kilio akishughudia uteketezaji wa kambi yake yenye vibanda 12, amekanusha kuwepo kwa chuo katika eneo hilo na kusema eneo hilo linatumiwa na wanafunzi hao kama eneo la mradi wa madrasa iliyopo katika kijiji cha Riroda kilichopo wilayani Babati, huku BAKWATA wilaya ya Hanang ikisema haikubaliani na ukiukwaji wa haki za watoto.

Video: CUF kwazidi kufukuta, utata mkubwa wagubika kesi yao
Video: Wanene Entertainment wadhamini tuzo ya ‘Video Bora’ tamasha la ZIFF