Kitendawili cha kuingia kambini kwa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa bado hakijateguliwa, kuafutia vikosi vya ulinzi la usalama kushindwa kujibu barua za maombi ya kuwaachia kwa muda wachezaji ambao wanaunda timu hiyo.

Rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa BFT Muta Lwakatare amesema tayari wameshaandika kwa mara ya pili barua za maombi kwa ajili ya wachezaji hao ili waingie kambini, lakini mpaka sasa hawajapatiwa majibu.

“Wachezaji hawa walilazimika kurejea katika vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kujiunga na timu zilizoshiriki michuano ya mkuu wa majeshi, na walifanya vizuri sana.

“Tunaamini majibu ya barua zetu yatatolewa wakati wowote kuanzia sasa, tunafahamu taratibu za vikosi vya ulinzui na usalama juu ya kuwaruhusu wachezaji hawa, hivyo hatuna haraka ya kusisitiza ili wawaachie.

“Vikosi vya ulinzi na usalama vimekua na mahusiano mazuri sana na BFT, hatuna shaka na hilo kabisa, wakati wowote wakiwapa ruhusa wachezaji, tutawapeleka kambini ili mambo mengine ya kuwaandaa yaanze mara moja.” Amesema Lwakatare

Lwakatare pia amezungumzi ujio wa kocha wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa kutoka nchini Kenya Mussa Oyombi, kwa kusema bado hajawasili jijini Dar es salaam, kutokana na kuchelewa kwa majibu ya kuruhusiwa kwa wachezaji.

“Kuwasili kwake kutatokana na kuruhusiwa kwa wachezaji, hawezi akaja hapa nchini wakati bado suala la ruhusa halijachukua nafasi yake, kwa sababu tunahofia gharama za kumuweka hapa Dar es salaam.”

Katika hatua nyingine Rais wa BFT amesema licha ya kuendelea kuchelewa kuanza kwa kambi ya timu ya taifa ya ngumi za ridhaa, bado Tanzania ina nafasi ya kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa ambayo ipo kwenye kalenda ya shirikisho la ngumi la kimataifa (AIBA).

Jaji Malecela wa Mahakama Kuu ya Tanzania aachia ngazi
Video: Polisi Dar wakamata watuhumiwa sugu wa ujambazi