Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa jumla ya watu 10 wamejeruhiwa huku 4 kati yao wakijeruhiwa vibaya, baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kukandamizwa na Kontena lilolobeba Tumbaku eneo la Nanenane.

Amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Agosti 17, 2020 majira ya saa 3:00 asubuhi, ambapo gari aina ya Costa iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro kulivagaa tela la lori lililokuwa limepata itilafu.

“Tela hilo lilikatika hivyo kusababisha Tela lililokuwa limebeba tumbaku kukata barabara yote na ndipo gari aina ya Costa iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam iliweza kuingia ubavuni kabisa mwa hilo Tela, tumeokoa jumla ya watu 6 wamepelekwa Hospitali na hali zao ni nzuri, lakini pia tumetoa watu 4 ambao walikuwa mbele kabisa na walikuwa wamekandamizwa na hali zao ni mbaya” amesema Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.

Ibada zarejea makanisani -DRC
Viongozi wa dini wakemea vurugu, matusi Uchaguzi Mkuu