Mbunge wa Jimbo la Segerea kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Bonnah Kamoli ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutekeleza ujenzi wa Barabara za kisasa kwa kiwango cha Lami katika Kata za Kiwalani na Minazimirefu zilizopo Jimboni humo.

Akichangia makadilio ya bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 bungeni Jijini Dodoma, Kamoli amesema kuwa Mradi huo wa ujenzi wa Barabara za Lami, umeenda sambamba na ujenzi wa mifereji mikubwa ya kuzuia maji ya mvua wakati wa masika, taa za barabarani, bustani za kupumzikia pamoja na masoko ya kisasa ambayo ujenzi wake unaendelea katika kata hizo mbili.

Amesema kuwa awali mradi huo ulikuwa unasuasua tangu mwaka 2005 na kusababisha changamoto kubwa kwa wananchi kwakuwa mvua zikinyesha ilikuwa inasababisha madhara makubwa kwa jamii.

“Maeneo ya Kata za Kiwalani na Minazimirefu mwanzoni yalikuwa hayatamaniki, lakini kwasasa naipongeza Serikali hakika inafanya kwa vitendo,”amesema Kamoli

Pia, Kamoli ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la kuwalipa fidia wananchi waliopisha maeneo ambayo miradi inatekelezwa.

 

Video: Tahadhari kama hizi zisipuuzwe, Marekani wanasiri kubwa- Chadema
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 21, 2019