Kampuni za simu nchini huenda zikafungiwa kufanya shughuli zao iwapo zitashindwa kuuza asilimia 25 ya hisa kwa wananchi kama sheria inavyotaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ambapo amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, Mbarawa amesema kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoka) ya mwaka 2010, ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka huu, inazitaka Kampuni za Mawasiliano kuuza asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi hivyo itakayokiuka  kufanya hivyo itatozwa faini au kufutia leseni.

“Wanatakiwa kuwa na umiliki  wa watanzania usiopungua asilimia 25 ya hisa zote kwa kipindi chote cha leseni. kiasi cha hisa zisizopungua asilimia 25 kitapatikana kupitia soko la hisa na dhamana kadri ya sheria ya soko lahisa na dhamana ya Tanzania”amesema Mbarawa.

Hata hivyo amesema kuwa Kampuni hizo zinatakiwa kusajili uuzaji wa hisa katika soko la Hisa ili kutoa fursa kwa wananchi kununua hisa za kampuni hizo.

Dkt. Shein azipongeza Cuba na Oman
Hatima ya Lema kujulikana leo