Kiungo wa zamani wa klabu ya Young Africans, Thaban Skalla Kamusoko amewashauri Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kutoidharau timu ya Red Arrows katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumapili (Novemba 28) Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Kamusoko ambaye kwa sasa anakipiga Zesco United ya Zambia ametoa ushaurio huo, kutokana na kuifahamu vizuri Red Arrows ambayo amewahi kukutanano mara kadhaa katika Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Amesema Red Arrows sio timu kubwa lakini inacheza kitimu na haina staa kwenye kikosi chao kwa hiyo Simba SC inapaswa kuchukua tahadhari kubwa.

“Red Arrows sio timu kubwa na haina historia kubwa ipo daraja la kati lakini inacheza kitimu, haina staa wachezaji wote wanajituma kwa hiyo Simba SC inapaswa kuchukua tahadhari kubwa.”

“Lakini kwa ukubwa wa Simba SC na uzoefu kwenye mashindano haya nawapa nafasi zaidi,” amesema Kamusoko ambaye ni rais wa Zimbabwe.

Simba SC iliangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa Ligi Mabingwa Barani Afrika kwa kufungwa na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Madaktari watakiwa kuzingatia maadili ya Taaluma
Nondo za Mwana Fa, kukwama kwa muziki wa Bongo